Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, December 24, 2012

Nigeria yaimarisha usalama kabla ya Krismasi


Nigeria yaimarisha usalama kabla ya Krismasi
Vikosi vya usalama vya jeshi la Nigeria vimeimarisha usalama nchi nzima kwa kuhofia mashambulizi ya wanamgambo wa Boko Haram wakati wa sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
Maafisa wa polisi wametakiwa kutokwenda mapumzikoni na kuimarisha usalama wa kiwango cha juu, huku harakati za watu zikipunguzwa na makanisa kulindwa.
Kwa miaka miwili sasa Nigeria imekuwa ikikumbwa na milipuko na mashambulizi yanayolenga makanisa wakati wa sikukuu ya krismasi. Ripoti zinasema kuwa mashambulizi hayo yanafanywa na kundi lenye misimamo mikali la Boko Haram.
Licha ya ulinzi huo kuimarishwa hasa katika miji ya kaskazini mwa Nigeria, Jumapili ya jana kulitokea mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga katika ofisi za shirika la simu za mkononi katika mji wa Kano ingawa hakuna mtu aliyeuawa au kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment