Wanajeshi wa Chad wakipiga doria katika mji mkuu N'djamena
Marekani imetuma vikosi vyake nchini Chad katika hatua ambayo inaonekana wazi ni kuzidi kujizatiti kijeshi barani Afrika.
Sababu iliyotajwa na Marekani ya kutuma
vikosi vyake nchini Chad ni wasiwasi wa Washington kuhusu usalama wa
raia wake kutokana na kuzidi kusonga mbele waasi katika nchi jirani na
Chad yaani Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Katika barua yake kwa maspika wa mabunge
mawili ya Marekani, Rais Barack Obama wa nchi hiyo amesema kuwa, raia
kadhaa wa Marekani wameondolewa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya
Kati, Bangui tangu tarehe 27 Disemba na hivi sasa kikosi cha wanajeshi
50 wa Marekani kimetumwa nchini Chad.
Watu wanaokosoa hatua hiyo ya Marekani
wanasema kuwa, hawaoni sababu ya Washington kutuma kikosi kizima cha
jeshi tena katika nchi ambayo haina machafuko kwa madai kuwa nchi jirani
ina machafuko hasa kwa vile tayari Marekani na Ufaransa zimekataa mwito
wa Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wa kusaidiwa
kukabiliana na waasi wa kundi la SELEKA.
No comments:
Post a Comment