Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, December 5, 2012

Mawakili wa Uamsho wakwama kufika mahakamani



NA MWINYI SADALLAH

Jopo la mawakili wanaowatetea viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, (Jumiki) limeshindwa

kufika mahakamani na kusababisha kesi hiyo kuharishwa hadi Desemba 17 mwaka huu.

Mawakili hao ni Salum Taoufiq, Abdalla Juma Mohamed na Suleiman Salum ambao wamekuwa wakiwatetea viongozi hao tangu kufunguliwa kesi hiyo Oktoba 21 mwaka huu.


Mwendesha mashitaka wa serikali

Ramadhani Abdallah, alisema kwamba pamoja na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika lakini upande wa mawakili wa utetezi wameshindwa kufika mahakamani na kuomba kupagwa tarehe nyingine ya
kutajwa kesi hiyo.

“Mheshimwa Hakimu upande wa mawakili wa utetezi hawajafika mahakamani hakuna taarifa yoyote kwa msingi huo tunaomba

mahakama yako kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kesi kwa sababu upelelezi bado kukamilika,” alisema.

Washitakiwa hao wanatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kupitia mawaidha ya mihadhara inayodaiwa kufanyika katika

msikiti wa Magogoni Msumbiji kati ya Agosti 17 na 18 katika Mkoa wa mjini Magharibi Unguja, kinyume cha sheria.

Kama kawaida viongozi hao walifikishwa mahakamani wakiwa chini ya ulinzi mkali

akiwemo Sheikh Farid Hadi Ahmed, Sheikh, Mselem Ali Mselem, Mussa Juma Issa, Azzan
Khalid Hamdan, Suleiman Juma Suleiman, Khamis Ali Suleiman na Hassan Bakari Suleiman.

No comments:

Post a Comment