Uturuki imekaribisha hatua ya
Muungano wa Kijeshi wa Nato ya kukubali kuweka makombora ya Patriot
kwenye mpaka wa nchi hiyo na Syria. Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki
imedai kuwa hatua zilizochukuliwa na Ankara kivyovyote vile hazina lengo
la kutekeleza hujuma yoyote ya kijeshi na kwamba lengo la kuweka ngao
hiyo ya makombora ni kwa ajili ya kulinda ardhi ya Uturuki.
Taarifa ya
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imeongeza kudai kuwa makombora ya anga
na ardhini ya Patriot hayatatumika kwa ajili ya kuasisi eneo
lisiloruhusu kuruka ndege huko Syria. Mawaziri wa Mambo ya Nje wa
Muungano wa Nato waliafiki ombi la serikali ya Ankara la kuweka aina
hiyo ya makombora katika mpaka wake na Syria katika kikao chao cha jana
huko Brussels Ubelgiji. Ngao hiyo ya makombora inatazamiwa kuwekwa huko
kusini mwa Uturuki katika kipindi cha wiki kadhaa zijazo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment