Mazungumzo kati ya serikali ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa mashariki mwa nchi hiyo
yanatazamiwa kufanyika wiki hii. Hayo yamesemwa na maafisa wa nchi
jirani na Kongo baada wa waasi wa M23 kuondoka katika mji wa Goma.
Maafisa wawili wa Uganda ambao wamekuwa wakijaribu kufanikisha
mazungumzo kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23 wamesema kuwa
pande mbili hizo zinatarajia kukutana Kampala Uganda wiki hii. Afisa wa
ngazi ya juu wa Kinshasa pia ameeleza kuwa ujumbe wa Kongo
unaowajumuisha wabunge na waziri mmoja unatazamiwa kuwasili Kampala wiki
hii kwa ajili ya mazungumzo hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment