
Vijana wengi wa Mali wametangaza kuwa wako tayari kujiunga jeshini ili kushiriki kwenye oparesheni za kukomboa maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo. Baada ya wanajeshi wa Mali kufanya mapinduzi tarehe 22 Machi mwaka huu makundi ya kabila la Tuareg na Ansaruddin tawi la mtandao wa al Qaida yalidhibti eneo la kaskazini mwa nchi hiyo na hadi sasa maeneo mengi ya kihisoria na kidini yameharibiwa na kubomolewa na makundi hayo yenye misimamo mikali huku raia wa maeneo hayo wakilazimika kuyakimbia makazi yao.
No comments:
Post a Comment