Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya
Marekani imeziondoa nchi tisa kwenye orodha ya nchi ambazo ilitishia
kuziwekea vikwazo iwapo zitafanya biashara na Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani imeeleza
kuwa, nchi hizo ni China, India,
Korea ya Kusini, Malaysia, Singapore,
Afrika Kusini, Sri Lanka, Uturuki na Taiwan. Taarifa hiyo imeonyesha
kuwa, nchi hizo ni wadau wakubwa wa kununua mafuta pamoja na kufanya
biashara nyingine na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.Wakati huohuo, Waziri wa Mafuta wa Iran amesema kuwa, biashara ya mafuta imevuka kwenye hali ngumu ya vikwazo na hivi sasa iko kwenye kilele cha ustawi. Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na Umoja wa Ulaya zinafanya njama za kuiwekea vikwazo Iran kwa madai kwamba Tehran inataka kutengeneza silaha za nyuklia, madai ambayo yamekadhibishwa mara kadhaa na viongozi wa ngazi za juu wa Iran na kusisitiza kuwa miradi ya nyuklia ya Tehran inafanyika kwa malengo ya amani.
No comments:
Post a Comment