Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka
watanzania kudumisha, amani, usalama na umoja. Rais Kikwete amesema hayo
wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika
hapo jana na kuonyesha kukerwa na watu wanaobeza maendeleo ya Tanzania.
Rais Kikwete amesema, wenye hila na chuki ndio wanaobeza maendeleo ya
Tanzania. Rais Kikwete aliyeongoza sherehe za uhuru wa Tanzania Bara
katika uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam amesema, nchi hiyo inatimiza
miaka hiyo ikiwa na amani, umoja na utulivu, lakini pia ikiwa imefanya
vizuri katika upande wa maendeleo ya kiuchumi. Aidha Rais Kikwete
alizitumia sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika
kutoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 3000 na kutoa Nishani ya Uhuru kwa
watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa na wasanii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment