skip to main |
skip to sidebar
Israel iliua watoto 41 katika vita vya Gaza
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadmau Amnesty
International limethibitisha kwamba watoto 41 wa Kipalestina waliuawa
katika mashambulizi ya siku 8 yaliyofanywa na majeshi ya utawala wa
Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza. Taarifa iliyotolewa leo na shirika
hilo imeeleza kuwa, maafa yaliyosababishwa na majeshi ya Israel katika
kipindi cha siku 8 ni makubwa zaidi kuliko mashambulizi yaliyofanyika
mwishoni mwa mwaka 2008 huko Gaza. Amnesty International imeeleza kuwa,
mauaji dhidi ya watoto katika vita vya utumiaji silaha, yanahesabiwa
kuwa jinai kubwa dhidi ya binadamu. Amnesty International imezitaka
kamati maalumu za Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na
asasi nyingine za kimataifa kuendeleza uchunguzi wao kuhusiana na
mashambulizi ya Israel dhidi ya raia wa Palestina wa eneo la Gaza.
Serikali ya Palestina iliyochaguliwa na wananchi na inayoongozwa na
Hamas imeeleza kuwa, mashambulizi ya siku 8 huko Gaza yalipelekea watu
185 kuuawa shahidi na wengine 1,399 kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment