Katibu Mkuu wa Chama cha Kiislamu cha Misri ametangaza kuwa Wamisri wanataka kufuata njia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Majid Ahmad Hussein Katibu Mkuu wa Chama cha Kiislamu cha
Misri amesema kuwa wananchi wa nchi hiyo wanataka kufuata njia ya
Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa Mashariki ya Kati ni eneo muhimu
ulimwenguni na kwamba Marekani inataka kumshinikiza Rais Mursi wa Misri
asiwasaidie Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza na aupatie utawala wa
Kizayuni gesi pamoja na kuudhaminia usalama.
Mwanasiasa huyo wa Misri ameendelea kusema kuwa adui mkubwa
wa mwamko wa Kiislamu si madikteta na wala vibaraka wao, bali ni
Marekani na Utawala wa Kizayuni.
No comments:
Post a Comment