Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, December 9, 2012

Vikosi vya AU vyadhibiti mji wa Jowhar Somalia


Vikosi vya AU vyadhibiti mji wa Jowhar SomaliaMajeshi ya Kulinda Amani ya Umoja wa Afrika na yale ya serikali ya  Somalia kwa pamoja yameuteka mji wa Jowhar nchini Somalia. Taarifa zinaeleza kuwa, mji wa Jowhar unahesabiwa kuwa ni mji mkubwa zaidi uliokuwa umesalia mikononi mwa kundi la wanamgambo wa al Shabab. Ali Houmed Msemaji wa Umoja wa Afrika nchini Somalia amesema kuwa,
amani na uthabiti umerejea baada ya kukombolewa mji wa Jowhar na wanamgambo wengi wa kundi hilo wameukimbia mji huo. Wakati huohuo, mawaziri watatu wa serikali ya Somalia wamenusurika kifo baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa al Shabab kwenye mji wa Merca ulioko umbali wa kilomita 100 kusini mwa Mogadishu. Inafaa kuashiria hapa kuwa, hapo jana vikosi vya serikali ya Somalia vilifanikiwa kuwauwa waasi  27 wa kundi la al Shabab na kuwajeruhi wengine 40 baada ya kutokea mapigano makali katika mji wa Bardera ulioko kusini mwa mkoa wa Gedo.

No comments:

Post a Comment