Waziri wa Ulinzi wa Misri ameyaalika
makundi yote kushiriki katika mkutano uliopangwa kufanyika leo huko
Cairo mji mkuu wa nchi hiyo. Meja Jenerali Abdulfatah al Sisi ambaye pia
ni Mkuu wa vikosi vya majeshi ya Misri ameeleza kuwa mkutano huo wa leo
hautazungumzia kuhusu siasa wala kura ya maoni ya katiba bali watakaa
pamoja kama Wamisri.
Kamati ya kisheria inayosimamia kura ya maoni
imeamua kwamba kura hiyo ya maoni inapasa kufanyika kwa muda wa siku
mbili badala ya siku moja. Kamati hiyo ilimuomba rasmi Rais Muhammad
Mursi kuwasilisha sheria inayoidhinisha kuwa kura ya maoni ifanyike
katika awamu mbili yaani Jumamosi ya tarehe 15 na Jumamosi ya tarehe 22
mwezi huu. Mapema jana raia wa Misri wanaompinga Rais wa nchi hiyo
walivuka vizuizi vilivyokuwa vimewekwa kwa ajili ya kuilinda ikulu ya
Rais huyo katika kuonyesha upinzani wao kwa rasimu ya katiba
iliyowasilishwa hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment