Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, December 2, 2012

Duni Haji apongeza kupungua maambukizo ya Ukimwi


Duni Haji apongeza kupungua maambukizo ya UkimwiWaziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Duni Haji amepongeza ripoti ya Umoja wa Mataifa inayoonesha kuwa kiwango cha maambukizo ya virusi vya Ukimwi kimepungua kwa asilimia kubwa katika nchi zilizoko chini ya Jangwa la Sahara na ametaka juhudi zaidi zifanywe ili kiwango hicho cha maambukizi kiende chini zaidi.
Akihutubia wananchi katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani hapo jana, Waziri Duni Haji alisema unyanyapaa bado unaendelea kukita mizizi miongoni mwa jamii ya Waswahili na ametoa wito kwa Wazanzibari kubadili mwenendo huo.
Ripoti ya UN inaonyesha kuwa kiwango cha maambukizo ya VVU kimepungua katika nchi masikini na kupanda katika nchi zilizoendelea hususan Marekani na nchi kadhaa za Ulaya.

No comments:

Post a Comment