skip to main |
skip to sidebar
Hamas iondolewa katika orodha ya magaidi
Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Bunge
la Iran amesema, kwenda sambamba malengo ya Hamas na Makubaliano ya
Umoja wa Mataifa kunalazimu kuiondoa harakati hiyo katika makundi ya
kigaidi. Nouzar Shafii ameashiria takwa la Ismail Haniya la kuondolewa
harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina katika orodha ya
makundi ya kigaidi na kuongeza kuwa, Wamarekani wameiweka harakati hiyo
kwenye orodha ya magaidi kutokana na sababu za kisiasa na kuunga mkono
kibubusa utawala wa Kizayuni wa Israel. Mbunge huyo wa Iran aidha
amesema kwamba falsafa ya kuundwa Hamas ni kupigania ukombozi na huru,
malengo ambayo ndio sura halisi ya makubaliano ya Umoja wa Mataifa na
kwa ajili hiyo basi Hamas inapaswa kundolewa katika makundi ya kigaidi.
Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Bunge la
Iran pia amekumbusha mashambulizi ya siku 8 ya Wazayuni dhidi ya Gaza
na kusema kwamba, harakati ya Hamas lililazimika kutumia silaha baada ya
kuzingirwa kikamilifu na Israel na haipaswi kuwekwa katika orodha ya
magaidi na makundi kama al Qaida na Taliban.
No comments:
Post a Comment