Mkuu wa Kamati ya Kupambana na
Mateso nchini Bahrain ameeeleza kuwa vitendo vya mabavu vya utawala wa
kifalme wa ukoo wa Aal Khalifa na kuwakandamiza raia wa nchi hiyo
vimebadilika na kuwa siasa za kila siku za utawala huo na kwamba bilaya
shaka yoyote siasa hizo haziwezi kudumu milele.
Rodney Shakespeare, Mkuu wa Kamati ya Kupambana na Mateso nchini Bahrain amemtaja Waziri Mkuu wa Bahrain ambaye kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita anashikilia wadhifa huo kuwa ndiye mhusika mkuu wa kuuliwa watoto, kutiwa mbaroni wanawake na kuteswa wafungwa huko Bahrain.
Amesisitiza kuwa utawala wa
Bahrain hauna mpango wa kuendesha uchaguzi wowote nchini humo kwa sababu
kufanyika uchaguzi wa aina yoyote nchini humo kutakuwa sawa na kuuondoa
madarakani utawala wa ukoo wa Aal Khalifa. Shakespeare amesisitiza
namna utawala wa Manama unavyopinga demokrasia na kueleza kuwa utawala
wa Aal Khalifa hatimaye utasalimu amri tu mbele ya matakwa ya
wananchi. Harakati za mapinduzi za wananchi wa Bahrain zilianza
Februari 14 mwaka jana na hadi sasa mamia ya raia wameuliwa, kujeruhiwa
na kutiwa nguvuni kufuatia mashambulizi ya vikosi vya Bahrain
vikishirikiana na vikosi vamizi vya Saudi Arabia dhidi ya raia
wanaoandamana.Rodney Shakespeare, Mkuu wa Kamati ya Kupambana na Mateso nchini Bahrain amemtaja Waziri Mkuu wa Bahrain ambaye kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita anashikilia wadhifa huo kuwa ndiye mhusika mkuu wa kuuliwa watoto, kutiwa mbaroni wanawake na kuteswa wafungwa huko Bahrain.
No comments:
Post a Comment