Muhammad Mahdi Aakif, kiongozi wa
zamani wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri ameukosoa msimamo wa
makundi ya kisiasa ya nchi hiyo wa kuyakataa matokeo ya awamu ya kwanza
ya kura ya maoni ya katiba na kusisitiza kwamba takwa la wapinzani hao
la kutaka kubatilishwa kura hiyo ya maoni halina msingi. Matokeo ya
awamu ya kwanza ya kura ya maoni ya katiba mpya ya Misri yanaonyesha
kuwa zaidi ya asilimia 56 ya wapiga kura wameunga mkono rasimu ya katiba
hiyo kulinganisha na asilimia 43 walioipinga. Kiongozi wa zamani wa
Ikhwanul Muslimin amesema msimamo wa mirengo ya kisiasa wa kung’ang’ania
takwa lao la kubatilishwa kura ya maoni na kuundwa baraza jengine jipya
la kutunga katiba mpya ya Misri haukubaliki. Awamu ya pili ya zoezi la
kura ya maoni ya katiba mpya ya Misri itafanyika siku ya Jumamosi katika
mikoa mingine 17, na matokeo rasmi ya kura hiyo yatatangazwa baada ya
awamu hiyo…
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment