skip to main |
skip to sidebar
Migodi 4000 ya dhahabu yagunduliwa Darfur
Waziri wa Madini wa Sudan ametangaza habari ya kugunduliwa migodi
4000 ya dhahabu huko Jebel Amir katika jimbo la Darfur ya Kaskazini
yenye uwezo wa kuzalisha tani 15 za dhahabu kwa mwaka sawa na kilo 70
kwa siku. Kamal Abdullatif amewaambia waandishi wa habari baada ya
mkutano wa baraza la mashauriano la Wizara ya Madini ya Sudan kwamba
wizara yake itaendelea kuzalisha madini hayo ili kuboresha uchumi wa
taifa.
Waziri wa Madini wa Sudan amesema kuwa mwaka jana uuzaji wa dhahabu
ulichangia pato la dola bilioni mbili la taifa na makampuni
yanayoendesha shughuli zake katika machimbo ya dhahabu yanatazamiwa
kufikia 15 hadi mwakani.
Kamal Abdullatif ameutaja uzalishaji wa dhahabu huko Jebel Amir kuwa
usio na kifani kwa kuwa vijana wengi wameacha na harakati za uasi na
kujishughulisha na uchimbaji madini.
No comments:
Post a Comment