Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa
hivi karibuni itatuma wanajeshi 140 nchini Somalia chini ya mwamvuli wa
Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika AMISOM. Kayode Aderanti
Afisa Mwandamizi wa Vikosi vya Kulinda Amani katika jeshi la Nigeria
amesema kuwa, wanajeshi hao wa Nigeria wanatumwa nchini Somalia kutokana
na makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya serikali ya Abuja na
Umoja wa Afrika. Nchi ya Somalia inashuhudia mapigano na machafuko tokea
ulipopinduliwa utawala wa Jenerali Muhammad Siad Barre mwaka 1991, kati
ya serikali ya mpito na makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka
likiwemo al Shabab. Umoja wa Afrika tokea mwaka 2007 uliunda kikosi cha
kulinda amani AMISOM kwa shabaha ya kuisaidia serikali ya mpito ya
Somalia kukabiliana na makundi ya waasi nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment