
Kundi la Kongresi ya Waislamu ambalo ni
taasisi ya kitamaduni ya Waislamu wa Kishia nchini Marekani ndiyo
imetisha maandamano hayo yatakayofanyika leo mjini New York.
Taasisi
hiyo imesema katika taarifa yake kwamba, Waislamu wa Amerika Kaskazini
watashiriki katika maandamano hayo kwa lengo la kupinga na kuzuia
kushtadi mashambulio dhidi ya Waislamu wa Kishia katika nchi za
Pakistan, Afghanistan, Iraq, Saudi Arabia, Syria na Yemen. Taarifa hiyo
imesisitiza kwamba, katika wiki mbili zilizopita mamia ya Waislamu wa
Kishia wameuawa kwenye nchi hizo.
No comments:
Post a Comment