Wawakilishi wa serikali ya Jamhuri
ya Afrika ya Kati na waasi wa Seleka wameafikiana juu ya kufanya
mazungumzo ya amani. Guy - Pierre Garcia Msaidizi wa Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika ya Kati amesema kuwa, wawakilishi
wa serikali ya Bangui na waasi wa Seleka hapo jana walikubaliana
kuanza kufanya mazungumzo bila ya masharti. Baadhi ya duru zinasema
kuwa, mazungumzo kati ya pande hizo mbili yenye lengo la kuleta amani na
uthabiti nchini humo yatafanyika tarehe 10 Januari mwakani huko
Libreville, mji mkuu wa Gabon. Waasi wa Seleka walianzisha operesheni
kamambe ya kijeshi wiki mbili zilizopita, na sambamba na kuteka miji
kadhaa walikuwa wanaukaribia mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment