Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
ameeleza kusikitishwa na kifo cha mwanachuo wa kike aliyekuwa akisomea
taaluma ya udaktari huko India, aliyefariki dunia baada ya kubakwa na
wanaume sita ndani ya basi la abiria lililokuwa katika mwendo. Msemaji
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Ban Ki Moon
amesikitishwa na kifo cha msichana huyo wa Kihindi na kutoa mkono wa
pole kwa familia na ndugu wa mhanga wa jinai hiyo. Ban Ki moon pia
ameitaka serikali ya India kuchukua hatua kali ili kuzuia kukaririwa
tena janga kama hilo huko India. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka
kupewa adhabu kali waliotenda jinai hiyo na kuwasaidia waathiriwa
wengine wa jinai kama hiyo huko India. Msichana huyo wa Kihindi
aliyekuwa na umri wa miaka 23 alivamiwa na kubakwa na wanaume sita
tarehe 16 mwezi huu na aliaga dunia jana akiwa hospitalini kwa matibabu
nchini Singapore.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment