Mwanamke mmoja wa Kibangladesh mwenye umri wa miaka 40, Monju
Begum, ameripotiwa kuukata uume wa mwanaume aliyedaiwa kujaribu kumbaka
na kisha kuvipeleka viungo hivyo polisi kama ushahidi.
Kwa mujibu wa polisi, mtuhumiwa huyo, Mozammel Haq Mazi, ambaye pia ni jirani wa Begum, alilazimisha kumdhalilisha kijinsia.
Wapelelezi wanasema kuwa Begum alikabiliana na shambulio hilo kwa
kuukata uume wa jamaa huyo kisha akaufunga katika kasha ya nailoni na
kuupeleka Polisi kama ushahidi kuwa Mazi alijaribu kumbaka.
Begum,
ambaye ni mwanandoa na mama mwenye watoto watatu, aliiambia Polisi kuwa
Mazi alikuwa akimsumbua kwa muda wa miezi sita. Ikaelezwa kuwa jamaa
huyo ana mke na watoto 5.
Msemaji wa Polisi, Abul Khaer,
anasema “Ni tukio la aina yake na lisilokuwa la kawaida kabisa .
Nijuavyo mimi, hii ni mara ya kwanza mwanamke anavileta polisi via vya
uzazi wa mwanaume kama ushahidi... Tutamkamata huyo mwanaume mara hali
yake itakapoimarika," alisema. Khaer.
Wakati huo huo, Mazi amekanusha tuhuma hizo na kuwaambia wapelelezi kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Mazi akasema "Hivi karibuni mwanamke huyo alishauri twende tukaishi
mjini Dhaka... Nilikataa na kumwambia kuwa siwezi kuwaacha mke na
watoto wangu, hivyo akalipiza kisasi."
Madaktari wanasema kuwa uume huo hautaweza kuunganishwa tena.
Wapelelezi wanasema kuwa Begum alikabiliana na shambulio hilo kwa kuukata uume wa jamaa huyo kisha akaufunga katika kasha ya nailoni na kuupeleka Polisi kama ushahidi kuwa Mazi alijaribu kumbaka.
Begum, ambaye ni mwanandoa na mama mwenye watoto watatu, aliiambia Polisi kuwa Mazi alikuwa akimsumbua kwa muda wa miezi sita. Ikaelezwa kuwa jamaa huyo ana mke na watoto 5.
Msemaji wa Polisi, Abul Khaer, anasema “Ni tukio la aina yake na lisilokuwa la kawaida kabisa . Nijuavyo mimi, hii ni mara ya kwanza mwanamke anavileta polisi via vya uzazi wa mwanaume kama ushahidi... Tutamkamata huyo mwanaume mara hali yake itakapoimarika," alisema. Khaer.
Wakati huo huo, Mazi amekanusha tuhuma hizo na kuwaambia wapelelezi kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Mazi akasema "Hivi karibuni mwanamke huyo alishauri twende tukaishi mjini Dhaka... Nilikataa na kumwambia kuwa siwezi kuwaacha mke na watoto wangu, hivyo akalipiza kisasi."
Madaktari wanasema kuwa uume huo hautaweza kuunganishwa tena.
No comments:
Post a Comment