
Akizungumza katika kikao baina ya timu yao na serikali huko Kampala, afisa huyo mwandamizi wa M23 amesisitiza kuwa, uongozi mbaya ndicho chanzo kikuu cha kutokea mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kufuatia tuhuma hizo ujumbe wa Kinshasa katika mazungumzo hayo umetishia kujitoa katika mazungumzo hayo. Waziri wa Ulinzi wa Uganda Crispus Kiyonga amethibitisha kujitokeza tofauti na mivutano hiyo hata hivyo amesisitiza kwamba, kuanza kwa mazungumzo hayo kumehuisha matumaini ya kupatikana suluhu baina ya pande mbili.
No comments:
Post a Comment