Mkuu wa Kamati ya Kupambana na
Vitendo vya Utesaji nchini Bahrain ameufananisha utawala wa Aal Khalifa
wa nchi hiyo na utawala wa Wanazi nchini Ujerumani na kuongeza kuwa,
Waziri Mkuu wa Bahrain ni mtuhumiwa nambari moja katika kuwauwa wanawake
na kuwatesa wananchi wa nchi hiyo. Amesema kuwa utawala wa Aal Khalifa
hauthubutu hata mara moja kuitisha uchaguzi huru nchini Bahrain, kwani
unajua wazi kwamba uchaguzi wowote utakaofanyika nchini humo utaung'oa
utawala huo wa kifalme. Ameongeza kuwa, Waziri Mkuu wa Bahrain ni mtenda
jinai nambari moja katika kuwauwa watoto,
wanawake, kuwafyatulia risasi
waandamanaji mjini Manama na kuwatia mbaroni wananchi na hatimaye
kuwatesa wakiwa korokoroni au gerezani. Mkuu wa Kamati ya Kupambana na
Vitendo vya Utesaji nchini Bahrain amezihutubu nchi za Magharibi kwa
kusema kwamba, nchi hizo lazima zielewe kwamba utawala wa Aal Khalifa
kwa kushirikiana na utawala wa Aal Saud wa Saudi Arabia zinakandamiza
demokrasia nchini humo. Amezituhumu pia tawala hizo kwa kuyasaidia
makundi ya kigaidi nchini Syria na hata zinaandaa mazingira kwa waasi wa
Syria kutumia silaha za kemikali nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment