Utawala wa Aal Khalifa wa Bahrain
unatumia hospitali kuwatesa wapinzani. Vijana wanaharakati wa haki za
binadamu huko Bahrain wameripoti kuwa utawala wa Aal Khalifa unatumia
baadhi ya hospitali kuwatesea wapinzani. Hospitali ya Suleimaniya ni
moja kati ya maeneo ambayo wapinzani hupelekwa kama majeruhi hata hivyo
wakiwa huko huteswa vibaya na vikosi vya usalama vya Bahrain. Taasisi ya
vijana watetezi wa haki za binadamu ya Bahrain imeashiria pia namna
wapinzani wanavyowekwa na kuteswa katika hospitali hiyo na kueleza kuwa
ghorofa ya kwanza na ya pili za hospitali hiyo zimetengwa makhususi kwa
ajili ya wagonjwa,
lakini ghorofa za juu za hospitali hiyo hutumika
kuwatia mbaroni na kuwatesa wapinzani wa utawala wa kifalme wa Aal
Khalifa. Hii ni katika hali ambayo wananchi wa Bahrain juzi walifanya
maandamano makubwa huko Manama mji mkuu wa nchi hiyo na kwenye miji
mingine na kutaka kung'olewa madarakani utawala wa Aal Khalifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment