Makumi ya waasi wamejisalimisha kwa
jeshi la Sudan. Mtandao wa habari wa Sudan Safari umeeleza kuwa, karibu
viongozi 22 wa kundi la waasi la "Mrengo wa Mapinduzi" na makundi
mengine ya waasi ambayo yanaendesha shughuli zao katika eneo la Abyei,
wameamua kuweka chini silaha zao na kujisalimisha kwa askari wa
serikali. Rahmat Abdur-Rahman, mmoja wa viongozi wa eneo la Abyei huko
kusini mwa Sudan, amenukuliwa akisema kuwa, viongozi hao wa waasi
wamethibitisha kuwa, makundi ya waasi hivi sasa yamedhoofika na yanazidi
kupoteza nguvu zao siku hadi siku. Kwa mujibu wa viongozi hao wa waasi,
wafuasi wengi wa makundi ya waasi wanataraji kujisalimisha hapo
baadaye. Abyei ni eneo la kusini mwa Sudan lenye utajiri mkubwa wa
mafuta, ingawa Sudan Kusini inadai ni mali yake na inawasaidia waasi
kupigana na serikali ya Sudan na kila anayeiunga mkono serikali ya
Khartoum.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment