Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, December 10, 2012

Waandamanaji 10 wauawa Sudan Kusini


Waandamanaji  10 wauawa Sudan Kusini
Kwa akali watu 10 wameuawa baada ya jeshi la Sudan Kusini kuwafyatulia risasi wakati walipokuwa wakifanya maandamano ya kupinga maamuzi ya serikali ya nchi hiyo. Liam McDowall  Msemaji wa Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini amesema kuwa,
jeshi la nchi hiyo limewafyatulia risasi na kuwauwa waandamanaji sita katika mji wa Wau makao ya jimbo la Bahrul Ghazal Magharibi. Ameongeza kuwa, waandamanaji wengine wanne waliuawa mapema hiyo jana. Waandamanaji hao walikuwa wakipinga uhamishwaji wa makao ya mkuu ya mkoa wa jimbo la Bahrul Ghazal Magharibi kutoka mji wa Wau na kuhamishiwa kwenye mji mwengine. Sudan Kusini ilijitenga rasmi na serikali ya Sudan mwezi Julai 2011, na kufanikiwa kupata majimbo 10 kati ya 25 na tokea kipindi hicho nchi hiyo imekuwa ikigubikwa na migogoro mingi kama vile harakati za waasi, mapigano ya kikabila, ukame na balaa la njaa.

No comments:

Post a Comment