Mufti wa Syria amesisitiza juu ya umuhimu wa kufanyika
mazungumzo ya kitaifa ili kuhitimisha mgogoro unaoikabili nchi hiyo.
Sheikh Ahmad Badruddin Hasun Mufti wa Syria amesema kuwa njama
zinazofanywa na baadhi ya nchi za Magharibi na Kiarabu dhidi ya Syria
zina lengo la kutoa pigo kwa utambulisho wa kiarabu na Kiislamu na
kuongeza kuwa njia pekee ya kujiondoa katika mgogoro huo ni kufanyika
mazungumzo ya kitaifa kati ya serikali na wapinzani wa nchi hiyo.
Sheikh Ahmad Badruddin Hasun amewaalika wapinzani wa ndani na nje ya
Syria kushiriki vilivyo katika mazungumzo ya kitaifa ya nchi hiyo na
kuwataka kuungana na wananchi na mfumo wa kiraia wa Syria ili kuilinda
nchi hiyo na mustakbali wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment