Serikali ya Tanzania imetishia kuishtaki kanali ya kimataifa ya
televisheni ya CNN kutokana na kanali hiyo kupeperusha habari zisizo na
uhakika kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa.
Habari hizo zilirushwa na kituo hicho nchini Marekani kuanzia Novemba 24-26 mwaka huu, ikionesha kuwa mpaka wa Tanzania upo ukingoni mwa ziwa hilo badala ya katikati.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene, amesema kituo hicho kilirusha vipindi vyenye upotoshaji na kutumia ramani isiyo sahihi. Amesema kutokana na upotoshaji huo, Serikali imechukua hatua ya kuuandikia barua uongozi wa CNN ili ukanushe habari hiyo mara moja. Ameongeza kuwa, mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi bado upo na hivi sasa umefikishwa katika Baraza la Marais 10 wastaafu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ili kuusuluhisha. Bw. Mwambene amesema kama mgogoro huo ukishindikana kupatiwa ufumbuzi katika baraza hilo, utapelekwa mahakamani.

No comments:
Post a Comment