Kwa uchache watu 10 wameuawa baada ya watu wanaobeba
silaha kushambulia Kanisa moja lililoko katika kijiji cha Chibok
kilichopo katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria. Kwa
upande mwengine, askari polisi wawili wameuawa kwenye shambulizi
lililofanywa na kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Shambulio hilo limefanyika katika eneo la Maiduguri lililoko umbali wa
kilomita 140 kutoka jimbo la Borno.
Taarifa zinasema kuwa, waasi hao wa
Boko Haram waliteketeza moto kituo kimoja cha polisi kilichoko katika
mji wa Gamboru Ngala jimboni humo. Hadi sasa mamia ya watu wameshapoteza
maisha yao na majengo kadhaa ya serikali na Makanisa kuchomwa moto
kutokana na mashambulio yanayofanywa na kundi la Boko Haram kaskazini
mwa Nigeria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment