Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, December 11, 2012

Waziri Mkuu wa Mali alazimika kujiuzulu


Waziri Mkuu wa Mali alazimika kujiuzulu
Waziri Mkuu wa Mali ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo masaa machache baada ya kutiwa mbaroni na wanajeshi wa zamani waliofanya mapinduzi nchini humo. Cheikh Modibo Diarra Waziri Mkuu wa Mali ambaye alitiwa mbaroni jana usiku na wanajeshi wafanya mapinduzi leo asubuhi ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo pamoja na baraza lake la mawaziri kupitia ujumbe alioutoa kwa njia ya televisheni.
 Wanajeshi wa Mali ambao tarehe 22 Machi iliyopita waliiengua madarakani serikali ya Amadou Tumani Toure kwa mara nyingine tena wamepelekea kujizulu Waziri Mkuu wa nchi hiyo kufuatia amri iliyotolewa na kiongozi wao Ahmadou Sanogo. Serikali ya Diarra imejiuzulu baada ya wanajeshi wafanya mapinduzi jana usiku kuivamia nyumba ya Waziri Mkuu huyo na kumtia mbaroni na baadaye kumpeleka katika kituo kimoja cha kijeshi.

No comments:

Post a Comment