skip to main |
skip to sidebar
Waasi wa Darfur wavamia nyumba za raia
Makundi kadhaa ya waasi katika jimbo la Darfur huko Sudan
yamekuwa yakipora na kuiba mali za raia na kuvisababishia hasara vituo
vya serikali. Makundi kadhaa ya waasi wa Darfur huko katika jimbo la
Darfur ya kaskazini nchini Sudan yamefanya hujuma hiyo dhidi ya raia wa
jimbo hilo na vituo vya serikali kwa kutumia magari 17. Othman Kabr
gavana wa jimbo la Darfur ya kaskazini pia ameeleza kuwa makundi ya
waasi wenye silaha yameshambulia pia huko kusini mashariki mwa jimbo la
Darfur ya kaskazini. Ameongeza kuwa waasi hao wamekuwa wakiwakwepa
wanajeshi walinda amani na kufanya mashambulizi katika maeneo ya raia na
kwenye masoko.
No comments:
Post a Comment