Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, December 4, 2012

Somalia yahitajia misaada ya kukabiliana na ukame



Somalia yahitajia misaada ya kukabiliana na ukame
Umoja wa Mataifa unahitaji kiasi cha euro bilioni moja kwa shabaha ya kukabiliana na balaa la njaa nchini Somalia.
Taarifa zinasema kuwa, Umoja wa Mataifa umeitaka jamii ya kimataifa itoe kiasi hicho cha fedha kwa shabaha ya kuisaidia Somalia katika kukabiliana na baa la njaa
litakalosababishwa  na ukame unaoinyemelea nchi hiyo kama ule ulioikumba mwaka 2011 na kusababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu.
Hili ni takwa la kwanza kutolewa na umoja huo tokea ilipoanza kuboreka hali ya kiusalama kwa kiasi fulani nchini Somalia. Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, watu wasiopungua milioni tatu na laki nane wanahitajia misaada, kwani mgogoro wa kibinadamu nchini Somalia ni moja kati ya migogoro hatari sana ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment