Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, December 31, 2012

Waasi wa A.ya Kati kufikiria kugawana madaraka


Waasi wa A.ya Kati kufikiria  kugawana madaraka
Waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekutana na Mwenyekitiwa  Umoja wa Afrika na kusema kuwa wako tayari kuchunguza pendekezo lililotolewa na Rais wa nchi hiyo la kushiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa.
Msemaji wa muungano wa waasi hao wa Seleka amesema kwamba, hata hivyo lengo lao si kuingia serikalini bali ni kuwawezesha wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati  kupata maendeleo na kujitegemea.
Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya Kati jana alisema kuwa yuko tayari kugawana madaraka na viongozi wa muungano huo wa waasi na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Bozize alisema hayo baada ya kukutana na Thomas Yayi Boni,
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mjini Bangui.
AU inafanya jitihada za kuandaa mazungumzo nchini Gabon kati ya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na waasi wa nchi hiyo ambao wameteka miji kadhaa na wameweka kambi karibu na mji mkuu.

No comments:

Post a Comment