Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, December 4, 2012

Wamarekani wawanajisi wanawake wa Kiafghani



Wamarekani wawanajisi wanawake wa Kiafghani
Wakazi wa kijiji kimoja cha kaskazini mwa Afghanistan wamesema kuwa askari wa Marekani wamewanajisi wanawake kadhaa wakati wa msako wa nyumba kwa nyumba uliofanywa na askari hao katika nyumba zao.
Wakazi wa kijiji hicho wanasema tukio hilo lilijiri eneo la Chahar Bolak kwenye jimbo la Balkh ambako kikosi maalumu cha jeshi la Marekani kilifanya msako wa nyumba kwa nyumba.

Wakati wa msako huo askari wa Marekani walitenganisha wanaume na wanawake wa familia 15 na kuwanajisi wanawake kadhaa. Askari wa Marekani wanalaumiwa kwa kufanya vitendo vingi vya kikatili dhidi ya raia wa Afghanistan tangu mwaka 2001. Mwezi uliopita askari mmoja wa Marekani aliyehusika katika mauaji ya umati dhidi ya raia wa kusini mwa Afghanistan mwezi Machi mwaka huu, alikiri kwa mara ya kwanza mbele ya korti moja ya kijeshi nchini Marekani kwamba alihusika na jinai hiyo.

No comments:

Post a Comment