Nchi zilizoko katika eneo la kusini mwa Sahara Kuu huko kaskazini
mwa Afrika, zimegeuka kuwa moja kati ya masoko muhimu ya magendo ya
silaha ulimwenguni katika kipindi cha miongo ya hivi karibuni. Duru
zinasema kuwa, Marekani imekuwa kinara katika kulibadilisha eneo hilo
kuwa soko kuu la magendo ya silaha duniani. Duru hizo zimeeleza kuwa,
nchi za China na Russia nazo pia zimetumbukia kwenye mkumbo huo kwani
zinatoa mikopo kama inavyofanya Marekani kwa minajili ya kuuza silaha
zao katika eneo hilo. Silaha zinazouzwa kwa magendo katika eneo hilo la
Sahara Kuu zinaangukia mikononi mwa maeneo yanayokumbwa na mapigano ya
kikabila, na maeneo ambayo yanadhibitiwa na waasi kama vile Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Somalia. Taarifa
zinasema kuwa, silaha hizo licha ya kuchangia machafuko, huongeza hatari
ya kuibuka mapigano mapya ya ndani na nje ya mipaka ya nchi hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment