Waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekutana na Mwenyekitiwa
Umoja wa Afrika na kusema kuwa wako tayari kuchunguza pendekezo
lililotolewa na Rais wa nchi hiyo la kushiriki katika serikali ya umoja
wa kitaifa.
Msemaji wa muungano wa waasi hao wa Seleka amesema kwamba, hata hivyo lengo lao si kuingia serikalini bali ni kuwawezesha wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kupata maendeleo na kujitegemea.
Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya Kati jana alisema kuwa yuko tayari kugawana madaraka na viongozi wa muungano huo wa waasi na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Bozize alisema hayo baada ya kukutana na Thomas Yayi Boni, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mjini Bangui.
AU inafanya jitihada za kuandaa mazungumzo nchini Gabon kati ya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na waasi wa nchi hiyo ambao wameteka miji kadhaa na wameweka kambi karibu na mji mkuu.

No comments:
Post a Comment