Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania amesema kuwa, Tume ya Mabadiliko ya Katiba
imekamilisha hatua ya kwanza ya kukusanya maoni ya mtu mmoja mmoja nchi
nzima na kwamba, hatua inayofuata ni ya kukusanya maoni ya makundi
maalumu. Akizungumza kwa mnasaba wa kuwadia mwaka mpya wa 2013 Miladia,
Rais Kikwete amesema, Bunge la Katiba, litakaa Novemba mwaka huu
kupitisha mapendekezo ya Katiba Mpya. Rais Kikwete amesisitiza kwamba,
kama kila kitu kitakwenda kama inavyotarajiwa, Katiba Mpya iliyotokana
na maoni na matakwa ya wananchi itapatikana ifikapo mwaka 2014.
Wakati
huo huo, Rais Kikwete amewataka Watanzania kupanga uzazi na kueleza
kwamba, matokeo ya sensa iliyofanyika mwezi Agosti mwaka huu yanaonesha
kuwa, idadi ya Watanzania imefikia milioni 45 na hiyo ni ishara kwamba
ifikapo mwaka 2016 kuna uwezekano wa idadi hiyo kufikia milioni 51 jambo
ambalo linaweza kuwa ni mzigo kwa taifa, jamii na hata katika masuala
ya uchumi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment