Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, January 9, 2013

Watoto walemavu waongezeka Marekani



Watoto walemavu waongezeka MarekaniViongozi wa Idara ya Afya ya Marekani wametangaza kuwa, mtoto mmoja mwenye ulemavu na upungufu wa viungo huzaliwa kila baada ya dakika tano nchini humo.
Coleen A. Boyle Mkurugenzi wa National Center on Birth Defects and Delevopmental Disabilities (NCBDDD) huko Atlanta Marekani amesema kuwa, kila dakika nne na nusu huzaliwa mtoto mwenye ulemavu na tatizo hilo huchangia asilimia ishirini ya vifo vya watoto wachanga nchini humo. Coleen Boyle ameongeza kuwa, watoto wanaozaliwa wakiwa na ulemavu na upungufu wa viungo wanakabiliwa na hatari zaidi ya kupatwa na maradhi. Amesema kuwa, mmoja kati ya kila watoto wachanga 35 wanaozaliwa nchini Marekani, huzaliwa akiwa kilema.

Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa, unywaji sana wa pombe, utumiaji wa sigara na dawa za kulevya pamoja na ukandamizaji na mateso ya kimwili wanayopata akina mama wajawazito ndizo sababu kuu zinazochangia 

No comments:

Post a Comment