Askari wa Kenya akihudumu chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika nchini Somalia
Duru za habari kutoka Somalia
zinaarifu kuwa, askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika, wamewaua kwa
kuwapiga risasi raia saba wa nchi hiyo kwa bahati mbaya. Duru za habari
zinaarifu kuwa, mauaji hayo yalitokea jana katika operesheni za
kuwasaka wanamgambo wa ash-Shabab waliodhaniwa kwamba walikuwa
wamekimbilia katika shule moja na hivyo kupelekea raia saba kuuawa
wakiwamo watoto watano. Dhahir Amin Jisu mmoja wa wabunge wa Somalia
amenukuliwa akisema kuwa, wahanga wa mauaji hayo ni watoto walio chini
ya umri wa miaka 10 na kwamba tukio hilo lilitokea katika mji wa Liju
ulioko umbali wa kilomita 120 kutoka mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Vikosi vya Umoja wa Afrika viko nchini Somalia kwa shabaha ya kuisaidia
serikali ya nchi hiyo kupambana na wanamgambo wa ash Shabab ambao wana
lengo la kuing'oa madarakani serikali ya Mogadishu kwa tuhuma kwamba, ni
kibaraka wa nchi za kikafiri.
No comments:
Post a Comment