Wafanyakazi wa majumbani nchini
Tanzania wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuweza kuwakomboa dhidi ya
matatizo yanayowakabili licha ya kwamba sheria za kazi zinawatambua.
Hayo yamedokezwa na Ofisi ya Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa –ILO-
nchini Tanzania. Mratibu wa mpango wa misaada ya maendeleo katika ofisi
ya ILO nchini Tanzania, Anne-Marie Kiaga amesema changamoto hizo ni za
pande tatu yaani usimamizi wa sheria, waajiriwa wenyewe pamoja na
waajiri.
Bi. Kiaga amesema hata wakati huu ambapo ILO kwa kushirikiana
na serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali inaendesha utafiti wa kina
kufahamu idadi halisi ya wafanyakazi wa majumbani nchini Tanzania kuna
changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo kujitambua na hivyo kinachofanyika
ni kuelimisha umma. Ripoti mpya ya shirika la Kazi duniani, ILO kuhusu
hali ya wafanyakazi wa majumbani imeonyesha kupanuka kwa sekta hiyo huku
mazingira ya kazi yakiendelea kuwa duni hususan katika nchi
zinazoendelea. Ripoti hiyo imetoa mfano na kusema nchini Tanzania
wastani wa saa za kazi kwa wafanyakazi wa majumbani kwa wiki ni saa 63
huku Austria ukiwa ni saa 15 kwa wiki, ilhali wastani huo unatakiwa uwe
kati ya saa 40 na 48 kwa wiki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment