Polisi nchini Afrika Kusini wametumia risasi za plastiki kujaribu
kuwatawanya wafanyakazi wa mashamba ambao wameitisha mgomo kutokana na
mishahara duni katika mashamba ya zabibu huko mkoa wa Cape Magharibi.
Jumatano hii mamia ya wafanyakazi wa mashamba hayo waliwarushia mawe polisi na kufunga barabara kadhaa kwa kuchoma moto matairi katika eneo hilo lililo kilomita 100 kutoka mji wa Cape Town.
Wafanyakazi hao wanataka mshahara wao wa dola nane kwa siku uongezwe maradufu. Vibarua hao ambao hufanya kazi kwa msimu kila mwaka hubakia bila ajira kwa miezi kadhaa baada ya kumaliza kazi zao.
Mwaka uliopita wa 2012 Afrika Kusini ilikumbwa na migomo kadhaa ya wafanyakazi waliokuwa wakidai nyongeza ya mishahara.

No comments:
Post a Comment