Ayatullah Mohsen Araki
Mkutano wa Kukurubisha Pamoja
Madhehebu za Kiislamu unatarajiwa kufanyika hivi karibuni hapa mjini
Tehran. Ayatullah Mohsen Araki Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukurubisha
Pamoja Madhehebu za Kiislamu ambaye yuko safarini mjini London Uingereza
amesema kuwa, mkutano huo utafanyika tarehe 28 na 29 za mwezi huu wa
Januari hapa mjini Tehran. Ayatullah Araki amesema kuwa, wageni kutoka
nchi 100 duniani wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo. Ameongeza
kuwa, mkutano huo utafuatilia mikakati na maazimio yaliyopasishwa katika
mkutano uliopita. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukurubisha Pamoja
Madhehebu za Kiislamu ameashiria mwamko wa Kiislamu katika ulimwengu wa
Kiarabu na kusema kuwa, Wamagharibi wanafanya njama za kuzusha fitina na
mifarakano baina ya Waislamu hivyo Waislamu wanapaswa kuwa macho na
njama hizo.
No comments:
Post a Comment