Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, January 29, 2013

Vikosi maalumu Tunisia katika viwanda vya mafuta


Askari wa Jeshi la Tunisia
Askari wa Jeshi la Tunisia
Kufuatia utekaji nyara wa hivi karibuni dhidi ya wafanyakazi wa kiwanda cha gesi huko nchini Algeria, Tunisia imetangaza kuwa imeweka askari wake maalumu kwenye taasisi zake za mafuta na gesi zilizopo kusini mwa nchi hiyo karibu na mipaka ya Libya na Algeria. Kamanda mmoja wa jeshi la Tuniasia ambaye hakutaka jina lake litajwe amenukuliwa akisema kuwa, hatua hiyo imechukuliwa tangu mwanzoni mwa wiki hii katika fremu ya kuimarisha vikozi vilivyoko katika maeneo ya jangwani kwa ajili ya kulinda usalama katika taasisi hizo. Kwa mujibu wa kamanda huyo, askari hao na zana kadhaa za kijeshi wamepelekwa kuimarisha doria katika maeneo ya Ramada na Dahabiya yaliyopo mpakani kati ya Libya na Algeria. Tangu Ufaransa ilipoanzisha mashambulizi yake huko nchini Mali makundi ya kigaidi ya eneo hilo yameanzisha mashambulizi ya kuyalenga maeneo nyeti kama vile viwanda,
kwa lengo la kuzilazimisha nchi vamizi hususan Ufaransa kusitisha uvamizi wao katika maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment