Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, January 22, 2013

Jeshi la Uganda lamuuwa mlinzi mkuu wa Kony


Jeshi la Uganda lamuuwa mlinzi mkuu wa KonyJeshi la Uganda limethibitisha kumuuwa mlinzi mkuu wa Joseph Kony kiongozi wa kundi la waasi wa Lord's Resistance Army (LRA).
Msemaji wa Jeshi la Uganda Kanali Felix Kulayigye amesema kuwa, Brigedia Binani ameuawa katika mapigano makali yaliyojiri katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati karibu na mpaka na serikali ya Sudan Kusini. Kanali Kulayigye ameongeza kuwa mapigano makali yanaendelea kati ya majeshi ya Uganda na waasi wa LRA katika eneo lililoko umbali wa kilomita 280 kaskazini mwa Diema.
Brigedia Binani anatuhumiwa kwa kutorosha watoto na kuwapeleka kwenye kundi hilo na wengine wakitumikishwa katika kukusanya chakula kwa ajili ya wapiganaji wa LRA. Inasemakana kuwa, nguvu za kijeshi za Kony zinazidi kupungua baada ya wapiganaji wake kupungua sana huku akijaribu kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine akikwepa mashambulizi ya majeshi ya Uganda katika maeneo ya mpakani ya nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini na Sudan.

Joseph Kony anapigana na serikali ya Uganda kwa zaidi ya miaka 20 sasa na anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) tokea mwaka 2005,  kujibu  tuhuma za kutenda jinai za kivita.

No comments:

Post a Comment