Kwa mara nyingine askari wa utawala wa Kizayuni umefanya
mashambulizi dhidi ya maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto
Jordan na kuwatia mbaroni Wapalestina wasiopungua 4. Duru za habari za
Palestina zinaarifu kuwa, jana pia askari hao walivamia mji huo na
kuwatia mbaroni Wapalestina 13 na kufanya idadi ya Wapalestina waliotiwa
mbaroni ndani ya kipindi cha siku mbili kuwa 17. Hii ni katika hali
ambayo, karibu kila siku askari hao huyavamia maeneo tofauti ya raia wa
Palestina na kuwatia mbaroni raia hao wa maeneo hayo. Ni vyema kuashiria
hapa kwamba, karibu Wapalestina elfu tano wanaendelea kuzuiliwa katika
jela za utawala huo. Wakati huo huo Khalid Mash'al, Mkuu wa Ofisi ya
Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas na Rais
Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina wanatazamiwa kukutana
hapo kesho mjini Cairo na kujadili kuhusiana na mazungumzo ya kitaifa
yaliyokuwa yakisuasua kwa miaka mingi. Duru za habari zimearifu kuwa,
tayari Khalid Mash'al amewasili leo mjini Cairo huku Abbas akitarajiwa
kuwasili nchini humo hapo kesho kwa ajili ya mazungumzo hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment