Watu wanne wameuawa na wengine
kadhaa kujeruhiwa kufuatia hujuma ya ndege isiyo na rubani ya Marekani
yaani Drone katika eneo la Waziristan Kaskazini nchini Pakistan.
Duru zinaarifu kuwa ndege hiyo
imevurumisha makombora manne katika nyumba moja na kusababisha maafa na
hasara mapema leo asubuhi.
Mara kwa mara ndege zisizo na rubani za
Marekani hutekeleza mashambulizi katika maeneo kadhaa ya Pakistan kwa
kisingizio cha kupambana na magaidi. Hata hivyo wahanga wakuu wa hujuma
hizo za Marekani ni raia wakiwemo wanawake na watoto wasio na hatia.
Marekani inatekeleza hujuma za ndege
zisizio na rubani katika nchi kadhaa za Kiislamu kama vile Afghanistan,
Yemen na Somalia kwa kisingizio hicho hicho cha kupambana na ugaidi
lakini wahanga wakuu huwa ni raia.
Wataalamu wa sheria za kimataifa wanasema hujuma hizo za ‘Drone’ ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
No comments:
Post a Comment