Watu 22 wameuawa na wengine 25 kujeruhiwa katika mapigano kati ya
raia na watu wenye silaha katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan.
Duru za habari zimemnukuu msaidizi wa gavana wa jimbo la Darfur Sediq
Abdel-Nabi kuwa, wapiganaji wa waasi wa Harakati ya Ukombozi
wanaoendesha shughuli zao za uasi nchini Sudan, walifanya mashambulizi
dhidi ya eneo la Zureiqat magharibi mwa wilaya ya Samaha katika jimbo
hilo na kuwateka nyara watoto watatu na wanawake 6. Kiongozi huyo
amesema kuwa, kufuatia tukio hilo, wakazi wa eneo hilo walijaribu
kuwakomboa mateka hao, hali iliyopelekea kuzuka kwa mapigano makali kati
yao na wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi na kupelekea watu 22 kuuawa
na wengine 25 kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wakazi wa eneo hilo waliivamia ngome ya harakati hiyo na kuibomoa sambamba na kuziteka ngawira silaha na zana za kivita za waasi hao. Sediq Abdel-Nabi ameitaka jamii ya kimataifa kuchunguza tukio hilo na kuilazimisha serikali ya Sudan Kusini kuheshimu mikataba ya kimataifa na kukomesha mashambulizi yake dhidi ya raia wasio na ulinzi wa jimbo hilo.

No comments:
Post a Comment