Rais Muncef Marzouki wa Tunisia
Serikali ya Tunisia imeonya
kuhusiana na taathira mbaya zinazoweza kulikumba eneo zima la Sahel na
nchi za magharibi mwa Bara Arabu kutokana na uingiliaji kijeshi nchini
Mali. Hayo yalisemwa jana na Rais Moncef Marzouki wa Tunisia ambaye
amesisitizia pia udharura wa kuimarishwa mawasiliano na mshikamano kwa
ajili ya kuitafutia ufumbuzi kadhia ya Mali. Katika ripoti hiyo
iliyotolewa baada ya kikao cha mawaziri wa ulinzi na wa mambo ya nje wa
nchi hiyo, imeelezwa kwamba,
mgogoro unaoendelea hivi sasa nchini Mali
ni hatari kubwa kwa nchi jirani ikiwemo Tunisia. Aidha ripoti hiyo
imesisitiza kuwa, Tunisia inaunga mkono umoja na amani wa taifa la Mali
dhidi ya makundi ya kigaidi. Aidha mawaziri wa Tunisia walilaani vitendo
vya utekaji nyara vilivyofanywa na makundi ya kigaidi huko kusini mwa
Algeria na kutangaza kuwa Tunisia iko pamoja na serikali ya Algiers
dhidi vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment