Aidha maandamano sawa na hayo yameripotiwa kufanyika katika mji wa Buraidah kaskazini kati mwa nchi hiyo.
Katika maandamano hayo yaliyofanyika Jumanne katika miji miwili, wananchi walitoa nara za kutaka upinduliwe utawala wa ukoo wa Aal Saud. Halikadhalika waandamanaji wametaka wafungwa wote wa kisiasa waachiliwe huru. Maandamano yameshadidi katika siku za hivi karibuni nchini Saudia hasa katika Mkoa wa Mashariki wenye utajiri wa mafuta ambapo kijana aliyekuwa akiandamana aliuawa shahidi Desemba 31.
Watawala wa Saudia ambao ni waitifaki wakubwa wa Marekani wamekuwa wakitumia mabavu kukandamiza maandamano ya amani ya wananchi. Walio wengi nchini Saudia wanataka uhuru wa kuwachagua viongozi wao pamoja na kukomeshwa dhulma na ubaguzi nchini humo. Maandamano ya wananchi huko Saudia yanafanyika katika fremu ya Mwamko wa Kiislamu ambao umekuwa ukishuhudiwa Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika
No comments:
Post a Comment